Msafiri, nyayo zako
Ndizo barabara, sio vinginevyo;
Msafiri, barabara haipo,
Hutengenezwa kwa kutembea.
Kwa kutembea watengeneza njia,
Na ukiangaza macho nyuma
Utayaona mandhari ambayo katu
Hutarudi kuyapitia.
Msafiri, hakuna barabara,
Bali mawimbi baharini.
ya Antonio Machado
imetafsiriwa na Wangũi Kamonji
Linapatikana hapa katika Kiingereza na Kihispania
Huku nikifanya juhudi ya kulitafsiri shairi hili katika Gĩgĩkũyũ kama unayo motisha ya kutafsiri katika lugha unayoizungumza wewe, nitumie utafsiri wako nitauchapisha hapa.