The past could not imagine me,
the present has not imagined me.
contemporary modern woman? Of course
I have to speak in correct
British English, exhaling
vowels and consonants
through my nose…roll my tongue…
Lakini wapi?
Hata hiyo mdomo ikijaribu
haiwesmake – na bila apology.
Walisahau kuambia nahodha,
lugha ilikuja ikimwagikanga kwa njia.
Na hii hatukuisave
ka petroli ya tanker Mombasa Highway imeanguka.
A-ah.
Hii tuka- finyanga, seremala, chomelea,
guzishia, nyongesea.
Ikawa yetu.
Hukuskia nguo ya kuombwa
haifunikangi rasa?
“ngumu kwangu Kizungu fluent
lakini huezi command umati nainfluence”
Juliani ‘Exponential Potential’
Talk to me