Tag: translation

msafiri hakuna barabara – machado in kiswahili

Msafiri, nyayo zako Ndizo barabara, sio vinginevyo; Msafiri, barabara haipo, Hutengenezwa kwa kutembea. Kwa kutembea watengeneza njia, Na ukiangaza macho nyuma Utayaona mandhari ambayo katu Hutarudi kuyapitia. Msafiri, hakuna barabara, Bali mawimbi baharini. ya Antonio Machado imetafsiriwa na Wangũi Kamonji Linapatikana hapa katika Kiingereza na Kihispania Huku nikifanya juhudi ya kulitafsiri shairi hili katika Gĩgĩkũyũ kama unayo motisha ya kutafsiri katika lugha unayoizungumza wewe, nitumie utafsiri wako nitauchapisha hapa.